The House of Favourite Newspapers

Global Habari Nov 25: JPM Ajitwisha Zigo la Makazi ya Wanajeshi

Rais DKT John Mafuli amefuta makato ya nyumba ambayo yalitakiwa yaanze kukatwa kwa wanajeshi kupitia Ngome allowance kutokana na mkataba ambao ulikuwa umesainiwa na serikali mwaka 2012/2013 huku akisema kuwa deni hilo litalipwa na serikali.

 

Rais Magufuli ameyasema hayo Wakati akiweka Jiwe La Msingi Ujenzi Wa Makao Makuu Ya Ulinzi Wa Taifa eneo lenye ukubwa wa Hekari 5366 lililopo Kikombo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Mkataba huo unaowataka wanajeshi kukatwa fedha kwa ajili ya kulipia nyumba walizojengewa kuwa ulisainiwa kimakosa.

 

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameliongezea Jeshi la Wananchi eneo ili kuweza kuimarisha ulinzi baada ya Mkuu wa Majeshi CDF Mabeyo kuliomba eneo hilo mbele ya Rais.

 

Hata hivyo Rais Magufuli Amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Dodoma kulipa fidia wananchi 1500 wanaostahili kulipwa kiasi cha Billion 3.399 kuanzia Dec Mosi Mwaka huu, huku akitoa onyo kwa wale ambao wameanza kupanga njama za kufanya utapeli.

Comments are closed.