The House of Favourite Newspapers

Udadisi, Ubunifu na Uvumbuzi wa Maarifa Mapya Unapotea kwa Uwepo wa Mtu/ Watu wa Kuigwa “Role Models”

2-pac

Watu ama mtu  mwenye kitu cha ziada katika jamii huigwa na wengine, watu hawa hutambulika kama kioo kwa wengine wajitazame hapo kutokana na ile ziada waliyonayo. Ziada hiyo yaweza kuwa ni mali, muonekano, maarifa au kipaji.

Uziada huo ndiyo unazalisha pande mbili ambazo ni muigwa na waigaji katika jamii fulani. Mtu mmoja anaacha kuishi maisha yake na kuishi maisha ya maigizo kumrejelea mtu wa mfano wake (anayeigwa).

Si jambo baya kuiga jema, waigaji wengi hawajui watu wanaowaiga wapi walianzia, tajiri huanza kuonekana baada ya kuupata utajiri na si kipindi anachoutafuta utajiri.

Ni makosa makubwa sana kuiga maisha ya mtu ambaye umeanza kuiona ile ziada yake inayomfanya aonekane katika jamii na si kuzingatia mizizi ya ile ziada yake imepatikana vipi.

LONDON, UNITED KINGDOM - JUNE 7: Bob Marley performs on stage at Crystal Palace Bowl on June 7th, 1980 in London, United Kingdom. (Photo by Peter Still/Redferns)

Wakati Mungu anakamilisha uumbaji wake alituwekea ziada ya asili, maarifa tofauti-tofauti ili tuweze kuujenga ulimwengu kila mmoja kwa nafasi yake. Mfanano wa maumbile si mfanano wa fikra, hivyo mtu mmoja kunakili maisha ya mtu mwingine kwa kujisemea “nataka kuwa kama mtu huyu”  si sahihi,  jambo sahihi ni kujisemea  kwamba” nataka kuwa zaidi ya mtu huyu”. 

Hii ni  kwa umakini mkubwa wa kuchambua mazuri na mabaya yake na kuzingatia utofauti uliopo baina ya muiga na muigaji  na  kuyatumia maarifa ya muigwa kwa kuongezea na ujuzi wa muiga (asili yako) ili kufanikisha kuleta jambo jipya ulimwenguni.

julius_nyerere

Ulimwengu unakosa mbinu mpya za kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu kwa kuwa na mfumo wa kumchagua mtu mmoja au kundi la watu na kuishi kama wao. Yaweza kuwa ni kwa baadhi ya nyanja au mfumo mzima wa maisha ya mtu kafanywa na mtu mwingine kwa makusudi kabisa ya kuiga.

Mungu alitufananisha sura pia kututenganisha mitatazo ili tuweze kuishi pamoja kwa kutegemeana. Hakuna mtu mwenye mawazo sawa na mwingine kiasilia bali usawa wa mazingira na mitaala ya elimu ya aina moja kwa watoto wenye vipaji tofauti mashuleni imezalisha kizazi chenye mtazamo wa aina moja na wigo wa fikra (fikra tegemezi).

Kwa nini hakuna bidhaa mpya? Kwa nini hakuna mawazo mapya? Kwa nini hakuna kizazi cha ubunifu badala yake kipo kizazi cha kunakili na kuyarudia yaliyokwishabuniwa? Kwa nini uwezo wa kufikiri unapungua siku baada ya siku?

Dunia imekuwa ileile ya kila siku yaani usiku na mchana, hakuna jipya badala yake vinajirudia vitu vilivyotendeka au vilivyobuniwa hapo awali na Waafrika tunabaki nyuma zaidi katika ulimwengu wa fikra na mawazo chanya. Waliotangulia walibuni vitu vingi tofauti ambavyo tunavibadilisha kulingana na mazingira kisha tunavitumia sasa.

michael-jackson

Benjamin Franklin katika karne ya 19 alikuwa ni mfanyabiashara maarufu Uingereza aliyewahi kuwa mfano wa kuigwa na wafanyabiashara wadogo. Wafanyabiashara hao wadogo ambao ni maarufu na walifahamika zaidi ni Thomas Mellon, B.F. Goodrich, na Frederick Weyerhauser,  ambao walimuiga hasimu wao katika biashara. Baada ya miaka kadhaa waigaji walikosa muelekeo baada ya Benjamin Franklin kuanza kutumia vilevi vikali vilivyopelekea mauti yake. Alitumia vilevi vikali kulingana na msongo wa mawazo uliotokana na mabadiliko ya biashara yake kuwa na utajiri mkubwa alioshindwa kuumiliki.

Uwepo wa utaratibu ya kuiga wengine unakinzana na falsafa ya hayati Mwalimu J.K.  Nyerere japo si moja kwa moja. Mtu anakuwa mtumwa kifikra kwa kuiga maisha ya mwingine, na zipo athari nyingi sana za kuwa na mtu anayemuiga mwenye tofauti za kiutamaduni na muigaji.

Limepotea kundi kubwa la vijana kwa kuwa na watu wa mfano wao katika maisha ambao wapo tofauti tofauti nao kimtazamo na muktadha wa mazingira.

Mfano kwa vijana wa Afrika hususani vijana wa Tanzania waliouchukua mfumo wa maisha wa hayati Tupac Omary Shakur wa Marekani, Bob Marley au Michael Jackson na watu wengine maarufu. Waliishia mwisho mbaya na wengine wamekosa muunganiko wa moja kwa moja kati ya mfumo wa maisha wanaoutumia na watu wanaowaiga.

Nihitimishe makala hii kwa kutoa hadhari za kuwa na hasimu katika maisha yako. Awali ya yote mawazo yako yatakuwa na mpaka yaani huwezi kwenda mbele zaidi ya hasimu wako, huwezi kuwa mbunifu, upekee hautokuwepo, utahusika moja kwa moja na changamoto zitakazomkumba hasimu wako na mwisho utaishi maisha yasiyokuwa yako.

Inashauriwa na wataalamu tusiwe na watu wa kuwageza bali tutumie maarifa ya watu waliochambua changamoto za maisha kisha tubuni njia mpya za kukabiliana na changamoto za maisha. Kila mtu katika nafasi yake atambue uwezo wake na kuleta suluhisho jipya la matatizo yaliyopo ulimwengu.

Ungana na mimi shemu ya pili ya makala hii itakayojadili namna ya kuwa mbunifu na jinsi ya kuyatekeleza mawazo mapya.

Salum Milongo.

GPL

halotel-1

Comments are closed.