The House of Favourite Newspapers

Breaking: Ajali Yaua 18 Kibiti Mkuranga

0

WATU 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahwewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, leo Jumatano, Aprili 15, 2020.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga, amesema ajali hiyo imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.

 

“Ni kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amesema Lyanga.

 

Amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam ilipogongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

 

Kamanda Lyanga amesema majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.

 

 

UPDATES: Idadi ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea Wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani leo asubuhi imeongezeka kutoka 18 na kufikia watu 21

 

 

Leave A Reply