The House of Favourite Newspapers

Abdul Nondo Ashinda Unenyekiti ACT Wazalendo

0

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), ambaye pia ni Mwanasiasa na mwanaharakati Abdul Omary Nondo ameshinda nafasi ya Uenyekiti Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo kwa kupata 61% ya kura zote zilizopigwa.

 

Mkutano huo wa uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Lamada, ulishuhudiwa na mgeni rasmi ambaye ni mwanaharakati na mwanasheria aliyewahi kuwa rais wa chama cha wanasheria Tanzania (TLS), Fatma Karume.

 

MAKAMU MWENYEKITI
Seleman Misango ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara) wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo.

 

Khadija Anwary Mohammed ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT wazalendo (Zanzibar).

 

Walioshinda nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu kupitia Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo:
1. Monalisa Joseph Ndala
2. Salim Mohamed Shafi
3. Mbaraka Chilumba.

 

Walioshinda nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu kupitia Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo:
1. Charles Paul Lowenge
2. Gora Shambuli Hamad
3. Hassan Abdallah Omar
4. Sharifa Mohamed Ali
5. Juma Haji Mmanga.

 

Mnamo mwaka 2018 Nondo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania wakati akiwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam kwa kipindi hicho, aliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na kupatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

 

Baada ya kupatikana alifunguliwa keshi yenye mashtaka mawili ambapo moja lilikuwa ni kutoa taarifa ya uongo kwa Afisa wa Polisi wa Kituo Mafinga akidai alitekwa na watu wasiojulikana na la pili ni kutoa taarifa za uongo mtandanoni kuhusu kutekwa kwake.

 

Mnamo Agosti 2018, alikutwa na kesi ya kujibu dhidi ya mashtaka hayo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Iringa. Novemba 2018 Mahakama hiyo ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia.

Leave A Reply