The House of Favourite Newspapers

LIVE: Wafuasi wa Chadema Wakinukisha Mahakani – “Tuueni tu”

0

VURUGU zimejitokeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya polisi kuwazuia watu waliokuwa wakitaka kuingia ndani ya chumba cha mahakama ili kusubiri muda ambao hukumu ya kesi inayowakabili viongozi wa Chadema utatolewa.

 

Ikiwa imebaki saa chache kusomwa kwa hukumu ya Vigogo wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Umati wa watu wakiwemo wafuasi wa Chadema umeendele kuongezeka. Aidha, Askari nao wameonekana wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.

 

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zanzibar Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicenti Mashinji, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche na Mbunge Bunda, Esther BULAYA.

LIVE: VURUGU ZAIBUKA MAHAKAMANI, HUKUMU YA MBOWE – “TUUENI TU”

Leave A Reply