The House of Favourite Newspapers

Adele Kununua Mjengo wa Rambo kwa Tsh Bil 133.7

0

IMERIPOTIWA kuwa, msanii maarufu duniani wa Pop, Adele Laurie Blue Adkins ‘Adele’ ametoa mkwanja kiasi cha takribani Dola za Marekani milioni 58 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 133.7 kwa ajili ya kununua jumba la kifahari la muigizaji nyota wa na mkongwe wa filamu za Hollywood, Sylvester Stallone maarufu kama Rambo lililopo Beverly Hills.

 

Adele yupo kwenye harakati za kulimiliki jumba hilo kubwa baada ya Rambo kupunguza bei kidogo kutokana na wateja kushindwa kumudu bei ya awali iliyokuwa imekifika hadi Dola milioni 110 ambazo ni sawa na Tsh Bilioni 253.6.

 

Rambo alinunua mjengo huo miaka ya 90 na alikuwa akiliuza jumba hilo kwa TSH.BILIONI 253.6, lakini tangu atangaze bei hiyo hakukuwa na mteja yeyote aliyejitokeza kununua hali iliyomlzimu kushusha bei hadi TSH. BILIONI 196 ambapo Adelel yeye amefikia bei ya Tsh Bilioni 133.7, hivyo huenda akafanikiwa kulinunua.

Leave A Reply