The House of Favourite Newspapers

Adele: Staa aliyezoa tuzo, asiyeishi kistaa

0

adele (4)Kwa jina lake kamili anajulikana kama Adele Laurie Blue Adkins. Ni Muingereza ambaye kwa kipindi kirefu cha nyuma alitamani kuwa staa mkubwa, alipambana na kutoa nyimbo kali kama First Love (2008), Make You Feel My Love (2008) na nyinginezo nyingi.

Hizo zote, hazikuweza kumtambulisha katika ulimwengu wa muziki mpaka pale alipotoa singo kali iliyobeba jina la Someone Like You ambayo ilimfanya kutambulika zaidi duniani na watu wote kutega masikio kwake, hapo ndipo ule umaarufu aliokuwa nao nchini Uingereza ulipozidi kuvuma kwa kasi ya upepo.

Watu wengi wamekuwa wakiufahamu wimbo huo zaidi ya wanavyomfahamu yeye mwenyewe. Adele ni nani? Alizaliwa wapi? Alitoa nyimbo zipi?

Majibu ya maswali hayo yote, utayapata hapa.

adele (1)Alizaliwa mwaka gani?

Adele alizaliwa tarehe 5 mwezi wa 5 mwaka 1988 huko nchini Uingereza. Kama ilivyokuwa kwa mastaa wengine hapa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na wengineo, naye Adele alilelewa na mzazi mmoja nchini Uingereza sehemu iitwayo Tottenham ambayo ipo Kaskazini mwa Jiji la London.

Ni lebo gani inayomsimamia

kwa sasa?

Wengi walitegemea kwamba Adele angeweza kusaini mkataba wa kufanya kazi na lebo kubwa nchini Marekani, lakini cha kushangaza, kwa kipindi chote, tangu anatoka mpaka sasa hivi, msanii huyu yupo kwenye lebo ambayo unaweza kusema ‘ndogo’ duniani iitwayo XL Recording ambayo ipo chini ya Prodyuza Richard Rusell.

adele (2)Analizungumziaje umbo lake?

Kwake, umbo si tatizo. Wengi walidhani kwamba baada ya kupata umaarufu labda angetengeneza umbo lake na kuonekana kama Beyonce au Celine Dion, ila aliamua kubaki na ubonge wake kwa muda mrefu. Hapa anasema:

“Ninapenda sana kula na ninachukia mazoezi. Sipendi kuonekana kwenye kurasa za mbele za majarida kama Playboy au Vogue. Nataka kuwa kwenye kurasa za mbele za majarida kama Rolling Stone au Q (Majarida yenye heshima)

Kwa nini alifuta ziara yake mwaka 2008?

Wakati alipanga kufanya ziara mwaka 2008 nchini Marekani, akaifuta. Wengi walilalamika kwani walimuhitaji sana. Alipoulizwa alisema kwamba katika kipindi hicho alichanganyikiwa kwenye uhusiano wake na mpenzi wake ambaye hakumtaja. Alikuwa na mawazo hivyo alijua kwamba kama angefanya ziara angevuruga, hivyo akaamua kuifuta.

adele (3)Someone Like You alimwandikia nani?

Wanamuziki wengi wanaandika nyimbo zao maalum kwa ajili ya mtu fulani au tukio fulani. Adele alipoulizwa sababu ya kuuandika wimbo huo alisema kwamba mwaka 2011 alikuwa akitoka na mwanaume mwenye miaka 30. Alimwamini sana, alimpenda na akajua kwamba angemuoa. Ghafla, akaachwa na mwanaume huyo kumuoa mwanamke mwingine kitu kilichomuumiza sana moyoni.

Mbali na maisha aliyopitia, misukosuko ya kimapenzi aliyoipata lakini muimbaji huyo amefanikiwa sana mpaka kuwa na utajiri unaokadiriwa kuwa dola milioni 80 (zaidi ya shilingi bilioni 160).

Ukiachana na Leona Lewis, BoB, Adele amekuwa mwanamuziki Muingereza aliyefanikiwa kwa kuchukua tuzo mbalimbali 86 kama Grammy, MTV Europe Music, Academy na nyingine nyingi.

Japokuwa amekuwa akikataa kuishi maisha ya kifahari kama wasanii wengine wenye majina, Adele amefanikiwa kununua nyumba nchini Uingereza ambayo ilimfanya kutoa mfukoni dola milioni 7 (zaidi ya bilioni 14).

Adele amekuwa mtu wa kujichanganya na watu wengi, huwa hajioni kama yeye ni staa, anasema kwamba kila siku anatamani kuishi kama alivyokuwa akiishi zamani, si mtu wa kujifungia ndani mara kwa mara. Anapenda kutoka mtoko na mpenzi wake aitwaye Simon Konecki na mtoto wake, Angelo James Konecki.

Baada ya kuvuma na wimbo wake wa Someone Like You na Skyfall ambao umetumika katika Muvi ya James Bond 007 ‘Skyfall’, Adela ameamua kutoka na wimbo mwingine uitwao Hello ambao umeanza kukimbiza kama kawaida yake.

Leave A Reply