The House of Favourite Newspapers

Aina tatu za kiharusi (Stroke)

0

stroke_hem_isoBaada ya kuona kinachosababisha kiharusi sasa tuone jinsi ugonjwa wa kiharusi ulivyogawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea, kwanza ni:

Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo kitaalam huitwa Ischemic Stroke. Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kusababisha tishu za ubongo za eneo lililoathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

 Hiki hutokea baada ya mshipa wa ateri kuziba kutokana na kuganda kwa damu, hali ambayo inasababisha damu isisafiri vyema na kuelekea kwenye ubongo.

Hali hiyo pia hufanya damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo  kitaalamu huitwa Cerebral Thrombosis au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo kitaalam huitwa Cerebral Embolism.

 Lakini tatizo hili linaweza kutokea pale damu inapoganda sehemu nyingine ya mwili na kusafiri hadi kwenye mishipa ya ateri, hivyo kusababisha damu kwenda kwenye ubongo kukwama.

Hata hivyo, tatizo hili linaweza kusababisha  kitu kinachoitwa Lacunar Stroke, yaani vimirija vidogovidogo sana vya damu vilivyopo ndani ya ubongo, vinaziba.

Hapo sasa binadamu huwa anakumbwa na kiharusi kinachojulikana kitaalam Lacunar Stroke japokuwa mara nyingi hii haiwaletei sana shida wagonjwa.

KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE

Baada ya kufafanua kiharusi kinachoitwa Ischaemia ambacho ndani yake tukaelezea pia kile kinachoitwa Lacunar Stroke sasa tuelezee aina ya kiharusi kiitwacho Haemorrhage.

Aina hii ya kiharusi mrija wa damu karibu ama kwenye ubongo hupata mpasuko, hivyo kusababisha damu kuvuja na kitendo hicho ndicho kitaalam huitwa Haemorrhage.

Kinachotokea ni kwamba damu inayovuja hukandamiza ubongo na kuuharibu, ubongo ni moja ya kiungo laini sana mwilini.

Katika hali ya kitaalam inayoitwa Intra Cerebral Haemorrhage, uvujaji wa damu hufanyika ndani ya ubongo wenyewe.

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply