The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu Amejibu “Mtoto Hana Baba, Majani Simjui” – Video

0

 

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amegoma kumuweka wazi baba wa mtoto wake ajaye huku akisisitiza kuwa sio P-Funk Majani ambaye watu wengi wamekuwa wakidai kuwa ndio baba wa mtoto wake.

 

 

Amber amesema hayo usiku wa kuamkia leo kwenye hafla ya Baby shower yake iliyofanyika pale Hekima Garden, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 

 

Wakati yupo kwenye ‘red carpet’ anafanya mahojiano na waandishi wa habari, Amber Lulu amesema anafuraha sana kuelekea kuwa mama mpya mjini ila cha ajabu hamfahamu ni mwanaume gani aliyempa ujauzito huo.

 

 

“Nijasikia vizuri kwa sababu naenda kuwa mama mpya mjini na kuna vitu vingi ambavyo vimebadilika na nahitaji kuvifanya, mimi mwenyewe baba wa mtoto simjui ila yupo na sio P Funk Majani, labda msubiri nikijifungua” amesema Amber Lulu.

 

Zaidi tazama tukio zima hapa chini kwenye video

Leave A Reply