The House of Favourite Newspapers

Ajibu, Mbappe waitwa Taifa Stars

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu (Kulia).

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amemuita mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu pamoja na staa wa Serengeti Boys, Kelvin John katika kikosi kitakachokwenda Misri katika michuano ya Afcon.

 

Amunike ameita kikosi cha wachezaji 39 ambao watafanya maandalizi kwa ajili ya kwenda Misri ambapo baadae atafanya mchujo ili kubaki 23 ambao watakwea pipa.

 

Amunike aliliambia Spoti Xtra jana kwamba kikosi hicho kimejumuisha wachezaji vijana ikiwa ni sehemu ya kuijenga timu ya taifa ya baadaye pamoja na maandalizi ya CHAN.

 

“Tunakwenda kwenye michuano hiyo tukiwa wapya kwa kuwa miaka 39 ni mingi, tunahitaji kuimarisha nidhamu na kujituma.

“Kikosi kitaingia kambini mwishoni mwa mwezi huu na ni vyema tukaingia mapema zaidi kwa ajili ya kufanya maandalizi mazuri, tunahitaji mechi mbili na timu ambazo zinashiriki michuano hii kupata uzoefu” alisema Amunike.

 

Walioitwa ni Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Mbao), Suleiman Salula (Malindi), Aron Kalambo (Prisons), Claryo Boniface (U-20), Hassan Kessy (Nkana), Vicent Philipo (Mbao) na Shomary Kapombe (Simba).

Gadiel Michael (Yanga), Abdi Banda (Baroka), Ally Mtoni (Lipuli), Mohammed Hussein (Simba), Agrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), David Mwantika (Azam) na Kennedy Wilson (Singida).

 

Feisal Salum (Yanga), Himid Mao (Petrojet, Misri), Mudathir Yahya (Azam), Yahya Zayd (Ismailia), Jonas Mkude (Simba), Ibrahim Ajibu( (Yanga), Fred Tangalu (Lipuli), Shaban Chilunda (Tenerife, Hispania), Frank Domayo (Azam), Shiza Kichuya (ENPPI) na Simon Msuva (Difaa).

 

Nyota wengine ni Rashid Mandawa (BDF), Mbwana Samatta (Genk), Thomas Ulimwengu (JS Saoura), John Bocco (Simba), Farid Mussa (Tenerife), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar), Miraj Athuman (Lipuli), Kelvin John (U-17) na Adi Yusssuf (Solihull Moors, England).

STORI NA KHADIJA MNGWAI |SPOTI XTRA

JPM: Mniamini Mimi MISHAHARA ITAPANDA | KIKOKOTOO Hata ULAYA Tunawazidi

Comments are closed.