The House of Favourite Newspapers

Anjella ‘Nilitaka Kunywa Sumu’

0

MSANII mpya kutoka lebo ya Konde Gang. Anjella amesema kuna wakati alitaka kutoroka na kunywa sumu kwani mama yake hakuwa akimsapoti kutimiza ndoto zake kimuziki.

 

 

Anjella amesema mama yake sio mtu ambaye anapenda muziki kwa sababu ni mtu wa kanisani lakini anamshukuru Mungu amesimamia malengo yake mpaka leo amefanikiwa kusainiwa Konde Gang.

 

 

“Nilimwambia mama watanikataza, watanipiga lakini msimamo wangu upo palepale kwa sababu sioni mafanikio yangu mengine nje ya muziki, kuna wakati nilitamani ninywe sumu na kutoroka nyumbani lakini nilituliza akili na kufuata mafundisho ya kanisani ambayo yalinisaidia,” amesema Anjella.

Leave A Reply