The House of Favourite Newspapers

Arsenal Wakosoa Uamuzi Laini wa VAR wa Kukataa Bao Lao Dhidi ya Manchester United

0
Arsenal wakosoa uamuzi wa VAR

KOCHA mkuu wa Arsenal Mikel Arteta na nahodha wa timu hiyo Martin Odegaard wamekosoa uamuzi wa kukataliwa kwa bao la Gabriel Martinelli katika mechi yao dhidi ya Manchester United.

 

Arsenal walipata bao la kuongoza dakika ya 12 ambapo Martinelli alimalizia vyema pasi Bukayo Saka baada ya Christian Eriksen kupokonywa mpira na Odegaard.

 

Lakini bao hilo lilikataliwa baada ya mwamuzi wa VAR Lee Mason kumshauri mwamuzi wa kati Paul Tierney kuangalia tukio la Christian Eriksen kupokonywa mpira na Odegaard ambapo aliamua kwamba Eriksen alichezewa vibaya na nahodha huyo wa Arsenal.

Ni laini mno, haikuwa faulo

Arteta anasema uamuzi wa kukataa goli la Martinelli ilikuwa ni ngumu kukubali, alisema”Ni ukosefu wa uthabiti. Ni laini wiki iliyopita, Aston Villa walipata bao wakati Aaron Ramsdale (Kipa wa Arsenal) alifanyiwa madhambi, lakini walisema ni laini na sio madhambi, kisha Bukayo Saka alifanyiwa madhambi na Tyrone Mings ndani ya box lakini ni laini na si penalti, leo hii ni madhambi”

Uamuzi wa kukataa goli la Martinelli ilikuwa ni ngumu kukubali

Odegaard anaamini alimkaba Eriksen kwa haki na bao lilipaswa kusimama, alisema “Kwa maoni yangu, kamwe sio faulo,”. Wikiendi iliyopita imekuwa na malalamiko mengi baada ya VAR kutawaliwa na maamuzi tata.

 

Imeandikwa na:John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply