The House of Favourite Newspapers

Arusha: Miili ya Watoto Wawili Yaopolewa Shimoni

0
Mashuhuda wa tukio hilo.

SAKATA la kutekwa kwa watoto wawili jijini hapa limechukua sura mpya baada ya jana miili miwili ya watoto kuopolewa shimoni katika eneo la Mji Mpya, Mtaa wa Olkerian.

Watoto, Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3), wakazi wa Kata ya Olasiti, Arusha walitekwa katika siku tofauti na hadi jana walikuwa hawajapatikana. Wakati Moureen alitekwa Agosti 21 saa kumi na moja jioni, Ikram alitekwa Agosti 26, saa 12 jioni.

Ingawa polisi hawakupatikana kuzungumzia tukio la kuopolewa kwa miili hiyo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari alisema alishuhudia uopoaji huo akisema kazi hiyo ilifanyika jana jioni.

“Nilipigiwa simu saa 11:32 nikitakiwa nifike eneo la tukio kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika ambako miili ilikuwa inaenda kuopolewa,” alisema.

Hata hivyo, hakutaka kuingia undani wa tukio hilo na kusema polisi ndiyo wanaoweza kulitolea maelezo tukio hilo.

Lakini baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutajwa walisema mwili mmoja unaoamini kuwa ni wa mtoto wa kiume ulikutwa ukielea ndani ya shimo la choo ambalo lilikuwa halijaanza kutumika na mwili mwingine unaodaiwa kuwa ni wa mtoto wa kike ulikutwa ukiwa umechinjwa na umefungwa kwenye kiroba.

Waandishi wetu walikuwa katika eneo la tukio lakini polisi waliwazuia kukaribia shimo hilo wakati uopoaji huo ukiendelea hivyo kulazimika kusimama mbali wakiwa na wananchi wengi waliokuwa wamejitokeza kushuhudia tukio hilo.

Mwandishi aliwaona askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo hilo.

Fuatilia LIVE Yanayojiri Bungeni Leo Septemba 6

Leave A Reply