The House of Favourite Newspapers

Polisi 4 Wafukuzwa Kazi Arusha – Video

0

 

POLISI  mkoani Arusha imesema kuwa polisi William Joseph, aliyekutwa na gongo, viroba, misokoto 20 ya bangi na kujiunganishia umeme nyumbani kwake kinyume cha utaratibu, amefukuzwa kazi kwa fedheha na jalada la kesi yake limepelekwa ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 7, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, ACP Salum Hamduni, ikisema kuwa tukio la polisi huyo kukutwa na vitu hivyo lilitokea Januari 5 mwaka huu mtaa wa Muriet jijini humo, mara baada ya mkuu wa wilaya hiyo, Kenani Kihongosi, na OCD kufanya msako na kumkuta na vitu hivyo.

 

Mbali na kukutwa na gongo, polisi huyo pia alikutwa na mafuta ya diesel lita 85, pakiti tatu za pombe aina ya kiroba, boksi 84 za viroba, ambavyo vilipigwa marufuku na serikali pamoja na kukutwa na vyuma vya bomba vilivyochakaa kinyume cha taratibu.

 

Mbali na hilo pia, polisi limewafukuza kazi polisi  wengine watatu, ambao walikamatwa kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Germs and Rocks Ventures iliyopo jijini Arusha, ambao ni G. 5134 DC Heavenlight Mushi, H.125 DC Gasper Paul na H.1021 PC Bryton Murumbe.

Leave A Reply