The House of Favourite Newspapers

Azam FC Yazitaka Pointi 3 za Gwambina

0

 

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, amefunguka kuwa maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya Gwambina FC unaotarajiwa kupigwa leo Jumatatu kwenye Dimba la Gwambina Complex, Mwanza, yamekamilika huku akitamba kuibuka na pointi zote tatu.

 

Azam FC imekuwa na mwenendo wa kusuasua kwenye mechi za hivi karibuni jambo lililopelekea kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Aristica Cioaba raia wa Romania na mikoba yake kupewa Mzambia, George Lwandamina.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Bahati amesema: “Maandalizi yetu kuelekea mchezo wa kesho yamekamilika, Gwambina ni timu nzuri, wana wachezaji wazuri na wazoefu.

 

“Tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili turudi kwenye mbio za ubingwa ambao ndiyo malengo yetu makubwa msimu huu.”

HUSSEIN MSOLEKA, Dar es Salaam

Leave A Reply