The House of Favourite Newspapers

Azimika kwa bia za chee

0

IMG_3759

Akiwa hoi baada ya kufakamia bia za bure.

Na Dustan Shekidele, Morogoro
KIJANA mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, Jumamosi iliyopita alijikuta akizimika baada ya kufakamia bia za chee, alizokunywa kwenye sherehe ya harusi iliyofanyika katika Ukumbi wa Glonency mjini hapa.

IMG_3740

….Akipewa maji ili kukata pombe.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kijana huyo baada ya kulewa, alianza kuwatapikia watu, hali iliyomlazimu MC wa shughuli hiyo, Nataris Nataris kuamuru atolewe nje, jambo lililotekelezwa na marafiki zake.

Walipomtoa nje, marafiki hao walimpa huduma ya kwanza kwa kumnywesha maji ya baridi ili kupunguza nguvu ya kilevi, lakini badala yake, kijana huyo alionekana kuzidiwa kwa kukosa nguvu na hivyo kukaa chini.IMG_3738Baada ya kuona mwenzao hakuwa na dalili za kuzinduka wenzake hao, walimtelekeza nje na kurejea ukumbini na kuendelea na sherehe.

Mmoja wa marafiki hao, aliyejitambulisha kwa jina la Juma Athumani alisema mwenzao huyo alifakamia bia kwa fujo huku akijua kuwa hakuwa amekula chakula.

Leave A Reply