The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kuhamishiwa Muhimbili, Rais Magufuli Amtembelea Kitwanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo Jumamosi, Februari 2, 2019 amemtembelea na mjulia Mbunge wa Jimbo la Misungwi ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa, juzi Alhamisi, Januari 31, 2019, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimuaga Mbunge huyo katika Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma akitokea katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini humo alipokuwa amelazwa na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Comments are closed.