The House of Favourite Newspapers

Baada Ya Kutua Lipuli, Busungu Alishukuru Championi

0
Kutoka kushoto ni Wilbert Molandi, (wandishi wa Championi na mchambuzi wa soka), Philip Nkini (mhariri na mchambuzi), Malimi Busungu na Saleh Ally (Mhariri Kiongzoi wa Championi) wakiwa kwenye Studio za Global TV Online baada ya kumalizika Kipindi cha SpotiHausi.

 

JUMATATU iliyopita aliyekuwa straika wa Yanga, Malimi Busungu alifanikiwa kujiunga na timu ya soka ya Lipuli ya mkoani Iringa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

 

Busungu alifikia hatua hiyo baada ya kupitia katika wakati mgumu wakati alipokuwa Yanga na kujikuta akipoteza matumaini ya kuendelea kucheza soka lakini baada ya uongozi wa gazeti hili kupitia cha mhariri wake mtendaji, Saleh Ally kuona hali hiyo alimkalisha chini na kupewa ushauri.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Busungu alisema: “Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata timu ya kucheza msimu ujao, pia nawashukuru sana wafanyakazi wote wa Championi hususan Saleh Ally kwa kazi kubwa aliyoifanya baada ya kupatwa na changamoto nyingi zilizotaka kunifanya niache kucheza soka wakati nilipokuwa Yanga.

 

“Kusema kweli alifanya kazi kubwa ya kunijenga kisaikolojia na kunipatia maneno ya ushindi ambayo alinitaka niyafanyie kazi, hakika namshukuru sana kwa hilo na nichukue nafasi hii kumwambia kuwa sitomwangusha tena nitafanya kama alivyonitaka nifanye ili niweze kufika mbali,” alisema Busungu.

VIDEO: SpotiHausi –Exclusive Interview na Malimi Busungu & Ivo Mapunda

Leave A Reply