The House of Favourite Newspapers

Baba kizimbani kwa kumlawiti mwanaye

0

NA Sijawa Omary, Risasi Jumamosi

MKAZI wa Kiyangu katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani mkoani hapa, John Nkondola (35), wiki iliyopita amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mtwara kwa madai ya kumlawiti na kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Peter Museti alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emily Mwambapa mahakamani hapo kuwa, tukio hilo lilitokeka Machi 25, mwaka huu ambapo mtuhumiwa anatuhumiwa makosa mawili ikiwemo la ubakaji ambapo alidai alimwingilia kimwili na kinyume na maumbile mtoto huyo (jina limehifadhiwa) kinyume na kifungu kidogo cha 130 (1), (2) (e) na kifugu 131(3) cha kanuni ya adhabu.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 83 ya mwaka 2006, mwendesha mashitaka huyo alitaja kosa la pili kuwa ni kulawiti mtoto huyo kinyume na kifungu namba 154 (a) na (2) cha kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
“Upelelezi wa kesi hii haujakamilika, hivyo mheshimiwa hakimu tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alisema mwendesha mashitaka huyo wa serikali.

Mtuhumiwa amekanusha mashitaka yote mawili na hakimu alimpa masharti ya kudhaminiwa kuwa awe na wadhamini wawili ambao watasaini dhamana ya shilingi 4,000,000 kwa maneno.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti na amepelekwa rumande na hakimu alisema kesi hiyo itatajwa tena Aprili 11, mwaka huu.

Leave A Reply