The House of Favourite Newspapers

Babab Levo: Mtaona Matusi ya Milioni 100

0

BABA Levo ni komediani na mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva waliotafuta njia ya tofauti ya kutoka kisanii na kujulikana sehemu mbalimbali.

Baba Levo amepita kwenye changamoto ya kuambiwa maneno yaleyale ya kukatisha tamaa, lakini alivumilia kila aina ya kashfa kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini alijua anataka nini hivyo amefanikiwa kumsinda shetani na kazi zake zote na sasa anakula matunda ya sanaa yake.

Sasa bana, wiki iliyopita, Baba Levo alilamba dili nono kutoka Active Media kama msemaji wao, jambo ambalo limemuweka kwenye ramani nyingine kipesa akiendelea kupishana na umaskini.

Baba Levo anasema kuwa, kwa sasa anakula anachotaka na siyo kinachopatikana kwa sababu ya pesa ndefu aliyolipwa aliyolipwa kiasi cha shilingi milioni 100 kwenye dili hilo.

Baba Levo amefanya mahojiano maalum (exclusive) na Gazeti la IJUMAA ambapo anafunguka juu ya ishu mbalimbali;

IJUMAA: Mambo vipi Baba Levo?

BABA LEVO: Salama kabisa, vipi hali, leta habari…

IJUMAA: Hongera sana kwa dili nono ulilopata…

BABA LEVO: Asante sana, watu wanatakiwa wawe na adabu sasa, ni msemaji wa kampuni kubwa mimi.

IJUMAA: Sasa kama ni msemaji wa kampuni kubwa vipi kuhusu mambo ya mitandao kujibishana na watu?

BABA LEVO: Hata hawa Active Media wenyewe waliniona huko kwenye mitandao na kunipenda hivyo sioni kama kuna tatizo. Kazi yangu inaendelea tu, mtu akikaa vibaya, ninamuweka sawa.

IJUMAA: Watu wengi wanajua wewe unapenda sana magari, sasa utaongeza gari lingine katika pesa uliyopata?

BABA LEVO: Magari ninayo ila tu nitatafuta moja kali zaidi kwa matumizi yangu mengine ya kibinafsi zaidi, najua mtaoni matusi yangu ya hiyo milioni 100.

IJUMAA: Mashabiki wako wangependa kufahamu umelamba dili la shilingi ngapi?

BABA LEVO: Hadi sasa hujapata habari? Maana hiyo ndiyo habari ya ya mjini. Nimepata shilingi milioni 100, kutoka Kampuni ya Active ambao ni mabingwa wa matangazo na masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini.

IJUMAA: Sasa wewe utakuwa unafanyaje kwenye kampuni hiyo?

BABA LEVO: Mimi ni msemaji mkuu wa kampuni hiyo kwenye taarifa mbalimbali zitakazohitaji kutolewa na Kampuni ya Active Media, ndiyo hivyo.

IJUMAA: Vipi kuhusu familia, lakini na mtoto wako mdogo?

BABA LEVO: Tuko salama kabisa, Mungu anatusimamia na hivyo tena tumelamba dili jipya, basi mambo yanakwenda safi.

IJUMAA: Vipi kuhusu wewe na Mwijaku, hivi mkikutana mnasalimiana kweli?

BABA LEVO: Yeye ndiye ananisalimia, siyo mimi maana ukweli ni kwamba tuko tofauti sana.

IJUMAA: Vipi kuhusu Harmonize maana wewe ni msanii na ukitaka hata kufanya naye kolabo itakuaje maana madongo unayoyarusha siyo ya kitoto?

BABA LEVO: Ila jamani…kwa hiyo unataka kunishusha tena mimi? Mimi kolabo nafanya na Diamond au huoni ile Shusha umeionaje lakini? Sitaki kusema sana ikawa matatizo hapa bure, maana unanijua sina vituo.

IJUMAA: Vipi kuhusu Shilole maana naona ukaribu umepungua siku hizi, kwa nini?

BABA LEVO: Ni ngumu kupungua, sema zamani nilikuwa naye muda mwingi, kumlinda na kipigo alichokuwa akikipata, lakini sasa hivi hali ni shwari kabisa.

IJUMAA: Nakushuru sana Baba Levo kwa ushirikiano wako.

BABA LEVO: Asante sana na karibu tena.

MAKALA: IMELDA MTEMA, BONGO

Leave A Reply