The House of Favourite Newspapers

Balozi wa Italia nchini Congo Afariki Katika Shambulio

0

 

 

BALOZI wa Italia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Luca Attanasio,  na watu wengine wawili, wamefariki katika shambulio lililofanya dhidi ya askari wa Umoja wa Mataifa kaskazini mwa mji wa Goma.

 

Shambulio hilo lilikuwa na lengo la kuwateka watu hao, na haikujulikana mara moja  wahusika wa mauaji hayo ambapo mmoja wa waliofariki alikuwa ni mwanajeshi aliyefuatana na balozi huyo.

 

Attanasio ambaye alikufa katika hospitali moja mjini Goma alianza kufanya kazi katika ubalozi jijini Kinshasa mwaka 2017 na hatimaye kuwa balozi kamili mwaka 2019.

Leave A Reply