The House of Favourite Newspapers

BASATA Yajitosa Video Chafu ya ‘Abdu Kiba’

0

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema wanalifuatilia suala la msanii Abdu Kiba linalomhusisha na kuvuja kwa video isiyokuwa na maadili katika mitandao ya kijamii.

 

Kupitia akunti ya mtandao wa Snapchat anayotumia msanii huyo, video hiyo imeonyesha akiwa na mwanamke wakiwa katika mapozi yaliyokosa maadili.

 

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Basata Geofrey Mngereza amesema; “Leo siku nzima nipo kwenye kikao na Cosota na video yake bado sijaiona lakini nawapa watu wangu waanze kuifuatilia, siwezi kudhibitisha au kuhakikisha kama ni yeye au sio yeye, lazima mtu uanze kufuatilia kwanza kisha tutoe majibu,” amesema Geofrey Mngereza.

EXCLUSIVE Steve Nyerere Afunguka Video ya Abdukiba ”Wapate Bakora”

Leave A Reply