The House of Favourite Newspapers

BATULI: MUNGU MKUBWA

0

 

 

AMA kweli Mungu mkubwa na hakuna kama yeye! Mwanamama sexy kunako Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, amesema kwa sasa yuko fiti tofauti na watu walivyokuwa wakisema ana hali mbaya.

 

Akizungumza na Celebrity Bongo ya Gazeti la IJUMAA juu ya afya yake baada ya hivi karibuni kuripotiwa kuwa hoi, Batuli amesema amegundua watu wanapenda kuona mtu anapata matatizo kisha kufurahia, lakini Mungu amesimama na yeye na sasa yupo okee kabisa.

 

“Mungu halali, ukweli ni kwamba alikuwa macho kwangu na hata sasa ananipigania. Sasa hivi niko fiti kabisa, namuomba Mungu azidi kunipa afya njema ili adui zangu waumbuke,” amesema Batuli ambaye aliibua taharuki kiasi cha baadhi ya kurasa za udaku mitandaoni kuzusha amekufa.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Leave A Reply