The House of Favourite Newspapers

Betika Lazidi Kuwapa Mchongo Wasomaji Wake

0

WASOMAJI wa gazeti la Betika maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam, wamesema   hawataacha kulichangamkia gazeti la hilo kwa sababu ndiyo suluhisho la matatizo yao.

 

 

Suluhisho ambalo wamelizungumzia  ni kushinda kirahisi wanapobeti mechi mbalimbali za soka zinazochezwa duniani.

 

 

“Gazeti hili linatupa pesa nyingi kwani kabla ya hapo tulikuwa tunabeti lakini kushinda inakuwa ngumu, hivi sasa ukisoma Betika kuna mbinu fulani ya kubeti unaipata na kurahisisha kazi yako ya kubeti,” alisema mmoja wa wasomaji  aliyejitambulisha kwa jina la Issa.

 

 

Betika linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na linaingia mtaani kila Jumatano.

 

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

 

 

Kila linapoingia mtaani, maofisa masoko wa Global Publishers hutembelea mitaa mbalimbali na leo Jumatano wametembelea manejo na Manzese na maeneo mengine.

 

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Antony Adam amesema heshima ya Betika inaendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

Leave A Reply