The House of Favourite Newspapers

Biden Awaondoa Wahouthi Kwenye Orodha ya Magaidi

0

SERIKALI ya Marekani inadhamiria kuliondoa kundi la waasi wa Kihouthi nchini Yemen kutoka kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

 

 

Afisa mmoja wa Ikulu ya White House amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kukabili moja ya majanga makubwa ya kibinadamu duniani.

 

 

Utawala uliopita wa Donald Trump uliliweka kundi hilo linaloungwa mkono na Iran kwenye orodha ya makundi ya kigaidi licha ya upinzani mkubwa wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada, ambayo yalisema kuwa hatua kama hiyo ingeliongeza ugumu wa kuwafikia na kuwasaidia raia waliokwama kwenye mapigano nchini Yemen.

 

 

Uamuzi huu wa umekuja siku moja tu baada ya Biden kutangaza kwamba Marekani inasitisha rasmi uungaji mkono wake wa vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen.

 

 

Mnamo mwaka 2015, utawala wa Barack Obama ambaye Biden alikuwa makamu wake, uliridhia kuanzishwa kwa kampeni hiyo ya kijeshi iliyodhamiria kuwazuwia Wahouthi kuendelea kutwaa udhibiti wa Yemen, ukiwemo mji mkuu wa Sanaa.

Leave A Reply