The House of Favourite Newspapers

Bob Junior Asalimu Amri Kwa Mondi

0

TAARIFA ikufikie kwamba lile bifu la kugombea jina la Rais wa Wasafi au Masharobaro kipindi hicho kati ya mastaa Bongo Fleva waliokuwa wakiibukia, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa prodyuza wake kunako Sharobaro Records, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, mambo yapo hivi.

 

Ni rasmi sasa kwamba, Bob Junior amesalimu amri kwa Diamond au Mondi kwenye sakata hilo.

Kipindi hicho, kila mmoja alidai yeye ndiye Rais wa Wasafi au Masharobaro kabla ya Bob Junior kupotea kimyakimya.

 

Lakini hivi karibuni, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limepiga stori na Bob Junior na kutaka kujua walivyomalizana. BOB Junior anasema kuwa, yeye na Mondi hivi sasa ni washkaji na hawana bifu lolote na ugomvi wa jina hilo alishamuachia Mondi muda mrefu.

 

“Mimi ndiye niliyekuwa Rais wa Masharobaro, lakini yote hayo yameshapita, hivi sasa tunaangalia mambo mengine, hakuna tena mtu mwenye bifu na mwenzake,” anasema Bob Junior.

 

Kuhusu ukimya wake, jamaa huyo anasema, ukimya huo una mshindo mkubwa kwani kuna mambo f’lani anayaweka sawa na kuwataka mashabiki wake kukaa mguu sawa.

STORI: RICHARD BUKOS

Leave A Reply