The House of Favourite Newspapers

ACT WAZALENDO YAITAKA SERIKALI KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA

Katibu wa Sera na Tafiti Ngome ya Vijana, Kitentya Luth,  akizungumza na waandishi wa habari.
Katibu wa Uenezi Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Karama Kaila akitoa ufafanuzi wa jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

CHAMA cha ACT- Wazalendo kupitia Ngome yake ya vijana imesema kuwa inasikitishwa na mwenendo uliopo hapa nchini  wa  ukosefu wa Ajira mpya na kutokuwepo kwa mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani hususani kwa vijana.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Sera na Tafiti Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Kitentya Luth ameiomba serikali kuweka mazingira rafiki katika kuhakikisha vijana waliopo mtaani kwa takribani miaka mitatu bila ajira kupata ajira, na kuwashirikisha katika uzalishaji mali.

 

Kitentya ameitaka serikali kupitia Waziri wa Viwanda, Waziri wa Ajira, Waziri wa Vijana na Waziri wa Fedha kukaa pamoja   ili kutafakari na kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara ndogo katika kuinua uchumi wa nchi na kuchochea Ajira.

 

Comments are closed.