The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: Mwalimu Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa Bukoba

Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemhukumu kunyongwa hadi kufa mwalimu Respicius Mutazangira kwa mauaji ya aliekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta, Sperius Eradius. Mwalimu Heriet Gerald aliekuwa akikabiliwa na mashtaka kama hayo ameachiwa huru.

Walimu hao walishitakiwa kwa kumuua kwa kukusudia Sperius Eradius aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo mwishoni mwa mwaka 2018.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi tisa katika kesi hiyo iliyosikilizwa kwa mwezi mmoja na Jaji Lameck Mlacha, ilianza Februari 6, 2019.

Inadaiwa walimu hao walitenda kosa la kumuadhibu kwa kipigo mwanafunzi Sperius Eradius kwa madai kuwa aliiba mkoba wa mwalimu  ukiwa na fedha.

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFAA: KESI YA DENTI BUKOBA

Comments are closed.