The House of Favourite Newspapers

Matokeo Darasa la Saba Yatangazwa, Yapo Hapa

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) imetangaza Matokeo ya Darasa la Saba uliofanyika Septemba 11, 2019 na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanya udanganyifu. 

 

NECTA imesema wamebaini walimu Wakuu, Wasimamizi na walinzi walihusika kufanya udanganyifu.

 

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ameyasema hayo leo wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba na kueleza kuwa katika kikao kilichokaa leo tayari wameshazitaarifu mamlaka za ajira na sheria ili ziwachukulie hatua waliohusika na udanganyifu huo. Ambapo kwa sasa udanganyifu kwa ujumla umepungua ambapo mwaka 2011 ulikuwa 9,736 na mwaka huu umefikia 900.

 

 

Dk. Msonde amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita.

 

Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi  Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar  es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.

 

“Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,” amesema Msonde.

 

BOFYA ====> PSLE-2019 EXAMINATION RESULTS

Comments are closed.