The House of Favourite Newspapers

Polisi, TCRA Watoa Ufafanuzi Kuhusu Uhalifu Mitandaoni

0
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa.

JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wametoa ufafanuzi kuhusu kushamiri kwa uhalifu wa makosa ya kimitandao.

Akitoa ufafanuzi huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa amesema kuwa wimbi la wizi wa fedha kupitia mitandao ya simu limeongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia huku akibainisha kuwa jeshi hilo linakabiliana na wahalifu hao ikiwemo kuwamakata na kuwafikisha kwenye vyovyomikono ya sheria.

Aidha, Mwakalukwa amewaasa wananchi kutoa taarifa polisi na siyo kwenda kulalamika TCRA wala kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa TCRA kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake, aliongea machache na kuwashurukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wao na pia kueleza changamoto mbalimbali zinazo wakabili pia alielezea historia fupi jinsi ya utendaji wao wa kazi na jinsi wanavyo yatatua.

 

Leave A Reply