The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: SIMBA YAIPIGA BAO YANGA, YAMSAJILI ERASTO NYONI

0
Erasto Nyoni.

 

Simba sasa ni kama imecharuka katika suala la usajili, baada ya Klabu ya Yanga kumuwinda kwa nguvu kubwa mchezaji kiraka Erasto Nyoni, hatimaye mchezaji huyo amesajiliwa na Simba.

Yanga ilikuwa ikimuwania mchezaji huyo aliyekuwa akiichezea Azam FC na ilielezwa kuwa tayari kulikuwa na mazungumzo baina ya pande mbili lakini Simba imemuwahi na kumsainisha mkataba wa miaka miaka miwili.

Taarifa kutoka Simba zinaeleza kuwa mchezaji huyo amesaini mkataba huo na sasa rasmi ni mchezaji wa Simba. Mchezaji huyo anasifika kwa kucheza nafasi nyingi uwanjani hasa za ulinzi wa kati na pembeni, pia mara kadhaa amewahi kutumika katika nafasi nafasi ya kiungo mkabaji.

Kwa sasa yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo inatarajiwa kucheza dhidi ya Rwanda, wikiendi hii katika mchezo wa marudio kuwania kufuzu michuano ya CHAN.

Leave A Reply