The House of Favourite Newspapers

Burundi Watua Dar, Watamba “Hatuwaogopi Stars” – Video

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Burundi kimewasili salama katika ardhi ya Tanzania kikitokea kwao Burundi kwa ajiri ya mechi ya marejeano kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Kikosi hicho kinatarajia kuumana tena na timu ya Taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) katika Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili ya Septemba 8, 2019, baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya bao (1-1).

Comments are closed.