The House of Favourite Newspapers

Cardi B Kuonekana Katika Fast & Furious 9

Kufuatia kiwango kizuri alichoonesha kwenye filamu ya Jennifer Lopez ‘Hustlers’ rapa Cardi B amepata nafasi nyingine kwenye kiwanda cha filamu nchini Marekani.

Staa wa filamu hizo ‘Vin Diesel’ alivujisha habari kwa kushea video katika akaunti yake ya Instagram
huku akiwa na rapa huyo.

 

Katika video hiyo Vin Diesel anasema” I’m tired, but I can’t wait” kuonesha shauku juu ya kazi hiyo mpya.

Huku Cardi B akidakia na kusema” I’m not gonna front, I think this is gonna be the best one” kujulisha
kuwa kazi kali inakuja. Ikumbukwe staa mwanamieleka John Cena naye amejumuishwa katika muendelezo wa filamu hiyo ya Fast & Furious.

Comments are closed.