The House of Favourite Newspapers

Carlinhos Akabidhiwa Majukumu ya Saido leo Mbeya

0

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa kurejea kwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Carlos Carlinhos kutaongeza ubora katika kikosi chake ambacho kitamkosa nyota Said Ntibazonkiza ‘Saido’ katika mchezo wao ligi kuu dhidi ya Mbeya City.

 

Yanga leo Jumamosi, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, wanatarajiwa kumenyana dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili kwa timu hizo.

 

Kuelekea katika mchezo huo kumbukumbu ya matokeo ya mchezo wa mzunguko kwanza kwa timu hizo kukutana, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na beki Lamine Moro huku pasi ya bao ikitolewa na kiungo Carlos Carlinhos.

Akizungumza na Championi Jumamosi, kocha Kaze alisema kukosekana kwa Saido katika kikosi cha Yanga ni habari mbaya lakini anaamini uwepo wa wachezaji bora wanaoweza kucheza katika nafasi yake kama Carlinhos utaisaidia timu hiyo kufanya vizuri.

 

“Saido atakosekana kutokana na kutokuwa fiti, hii si habari njema kwa Wanayanga wote kwa kuwa wanafahamu uwezo wa Saido, lakini naamini bado kuna wachezaji wazuri ndani ya Yanga ambao wanaweza kucheza na kuisaidia timu kufanya vizuri.“

 

Kuhusu Carlos Carlinhos nafurahi kuona amerejea katika kikosi, ni mchezaji mzuri ambaye pia hucheza katika nafasi ambayo hucheza Saido na akafanya vizuri, tunatarajia kupata ubora na huduma nzuri kutoka kwake kama ilivyo kwa wachezaji wengine wa Yanga ambapo muhimu kwetu ni kupata ushindi hivyo tutajitahidi kuhakikisha tunashinda,” alisema kocha huyo.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply