The House of Favourite Newspapers

China Yatangaza Ushindi Dhidi ya Coronavirus

0

SERIKALI ya China imesema kuna wagonjwa wapya 31 wa ugonjwa wa COVID-19 na vifo vinne hivi leo, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kamisheni ya Afya ya nchi hiyo.

 

Miongoni mwa wagonjwa hao 31, thalathini walitoka nje ya nchi hiyo, na ni mmoja tu aliyeambukizwa katika jimbo la kaskazini magharibi la Gansu.

 

Wanne waliofariki dunia ni kwenye jimbo la Hubei, chimbuko la maambukizi ya kirusi cha corona, ambalo hata hivyo halina mgonjwa mpya.

 

Jimbo hilo lililokuwa kwenye marufuku ya kutotoka nje, limeanza kurejea kwenye maisha yake ya kawaida.

 

“Maambukizi kutoka nje” ndicho kikwazo kikubwa kwa China kwa sasa, baada ya hapo jana Baraza lake la Taifa kutangaza kwamba kimsingi nchi hiyo imefanikiwa kuuzuwia ugonjwa wa COVID-19.

 

Tangu kirusi hicho kianze kusambaa mwezi Disemba mwaka jana, watu 81,470 wameambukizwa nchini China pekee, ambako 3,304 wamepoteza maisha.

 

***** TOP 5 *****

1. United States  – 142793 cases – 2490 deaths

2. Italy – 97689 cases – 10779 deaths

3. Spain – 85195 cases – 7340 deaths

4. China – 81470 cases – 3304 deaths

5. Germany – 62435 cases – 541 deaths

Last updated: March 30, 2020, 12:29 GMT.

Leave A Reply