The House of Favourite Newspapers

Chris Brown kumshtaki promota Mfilipino

0
Mwanamuziki Christopher Maurice ‘Chris Brown’

 

STAA wa Muziki wa R&B, Christopher MauriceChris Brown’ amejipanga kumshtaki promota kutoka Ufilipino, Jose Victor Los Banos kwa kujichukulia pesa kiasi cha dola 300,000 (zaidi ya milioni 660 za Kibongo) kwa njia ya utapeli.

Kwa mujibu wa ripoti, Chris ameamua kufikia uamuzi huo baada ya kugundua kuna mipango ilipangwa kuchukua pesa hizo ambazo alizilipa miaka mitatu iliyopita.

Ilikuwa hivi; Chris aliandaliwa shoo nchini Ufilipino katika Sikukuu ya Mwaka Mpya 2014 lakini hakutokea kwa sababu binafsi, badala yake aliomba kuirudia Julai 2015 ambapo-alipa-ngiwa ratiba na kuifanya ndani ya muda.

Anacholalamika Chris, baada ya kumaliza shoo hiyo akiwa hotelini akijiandaa kuondoka nchini humo alifuatwa na promota huyo na kumdai kiasi hicho cha pesa na kumwambia sababu ilikuwa kuingia mitini shoo ya kwanza ya 2014 na kuishinikiza idara ya uhamiaji kumzuia hadi atakapolipwa jambo lililotekelezwa.

Kwa sasa, Chris amefungua mashtaka hayo (haijatajwa mahakama) na kulalamika alipwe fidia.

INSTALL GLOBAL PUBLISHERS APP sasa usipitwe na matukio
PAKUA HAPA==>GLOBAL PUBLISHERS APP

FULL VIDEO; Mapambano Ngumi za Global TV – Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania Bingwa

Leave A Reply