The House of Favourite Newspapers

Barakah The Prince: Alikopita Ameacha Shida!

1
Barakah The Prince.

 

JINA Barakah The Prince si geni kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Ni miongoni mwa wasanii wa R&B wanaofanya vizuri. Ngoma iliyomtobolea tobo ni Jichunge kisha Siachani Nawe, Nivumilie, Siwezi na Nisamehe. Hadi sasa, ameshapiga shoo kibao ndani na nje ya nchi sambamba na kolabo zisizokuwa na idadi Bongo.

Licha ya kufanya huko vizuri, nyuma yake amepitia vitu vingi, ameacha shida nyingi katika kila menejimenti anayokuwa nayo. Kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2017 tayari ameshatemana na menejimenti kubwa tatu na kuacha shida.

Katika makala haya yanachambua zaidi;

Tetemesha Entertainment

Ilikuwa ni lebo ya kwanza chini ya Kid Bway kumuona Barakah kama msanii chipukizi na kumsainisha mwaka 2013 akitumia jina la Barakah Da Prince. Katika lebo hii ambayo ilianza rasmi 2012 jijini Mwanza, imefanikiwa kuwatoa wakali kibao akiwemo Hussein Machozi, Sajna na C-Sir Madini.

Alikiba.

 

Baada ya Barakah kusainishwa 2013, mwaka mmoja baadaye ilitambulisha ngoma zake ikianzia na Jichunge kisha Siachani Nawe na nyinginezo.

Hakudumu nayo, 2015 aliacha shida Tetemesha baada ya kuondoka bila taarifa na kuhamia lebo nyingine ya kuandaa na kusimamia muziki ya Royal Nsyepa.

Katika moja ya mahojiano yake juu ya sababu za kuhama, Barakah anasema;

“Nimemwambia mara kibao Kid Bway juu ya kuondoka kwangu akawa hajibu meseji sa’ mi ningefanyaje wakati muda unazidi kwenda hakuna kinachotendeka katika kazi zangu.

“Hii ni kazi naangalia kwenye masilahi siwezi kung’ang’ania sehemu ambayo haina masilahi.”

Lakini alipotafutwa Kid Bway alilalamika kutopewa taarifa ya Barakah kuhama.

Royal Nsyepa

Alipotinga katika lebo hii mwanzoni mwa 2015, Barakah alisaini mkataba wakati akijua ule wa Tetemesha bado hajamalizana nao.

Hata hivyo, Royal walikuja kumalizana na Tetemesha baada ya misukosuko ya hapa na pale na kuanza kufanya kazi na msanii huyu ambapo ngoma kama Siwezi iliweza kusimamiwa vyema kuanzia audio mpaka kichupa.

Wakati mashabiki na uongozi wake huo ukiamini wanaweza kufika mbali, Barakah aliamua napo kuacha shida kwa kujiunga na lebo nyingine ya Rockstar4000.

Lady Jaydee ‘Jide’.

 

Kwa mujibu wa meneja Royal Nsyepa katika mahojiano alisema;

“Barakah amekuwa mtovu wa nidhamu, kafikia hatua ya kutuandikia barua ya kutaka kusitisha mkataba wakati sisi ndiyo tumemfikisha hapo alipo. Tumeamua kuachana naye!”

Kama ilivyo kwa tetemesha, Royal iliamua kujiweka pembeni na kumuacha Barakah akiingia Rockstar4000 na kubadilishwa jina la Barakah Da Prince kuwa Barakah The Prince.

Rockstar4000

Julai 2016, Barakah alithibitisha kuwa mmoja wa memba wa Rockstar4000 akiungana na Lady Jaydee pamoja na Ali Kiba.

Moja ya mafaniko aliyoyapata akiwa ndani ya Rockstar4000 ni kuzunguka nchi mbalimbali Afrika kufanya ‘interviews’ na kujifunza, mipango ya kolabo na wakali kutoka Angola, Kenya na Afrika Kusini sambamba na kutoka na video kali akiwa na Ali Kiba ya Nisamehe.

Licha ya kuwepo kwa yote hayo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Barakah aliacha shida nyingine baada ya kutangaza kujitoa katika lebo hiyo na kuhamia kwenye lebo yake mwenyewe ya Bana Music aliyoianzisha kwa kushirikiana na mpenzi wake, Najma Dattan.

Baraka amenukuliwa akisema;

“Nashukuru na siwezi kusahau waliponisapoti kutoka ngazi moja kwenda nyingine. Itambulike sasa hivi sipo chini ya mtu yeyote yule, mtu atakayekuja kunidis kwa nini nimetoka Rocklstar4000 hiyo hainihusu, wakati mwingine siyo unaangalia sana nani ataongea nini. Sipendi kusifiwa kwa vitu ambavyo havipo.

“Nataka kufika sehemu, mpaka nasaini Rockstar4000 nilikuwa na mipango yangu kwa hiyo kama sioni ikifanyika naondoka.”

Bana Music

Kwa sasa amejikita katika lebo yake ya Bana Music akishirikiana na mpenzi wake, Najma Dattan. Barakah anasema;

“Najua nateseka kiasi gani, mashabiki wanalalamika sana hawanisikii. Sina budi kutangaza rasmi kabisa kuwa Barakah sipo chini ya Rockstar4000 sipo chini ya mtu yeyote na haitakuja kutokea labda itumike nguvu sana.

“Kuanzia muda huu, Barakah kazi zake zinafa-nywa na Bana Music.”

Makala: Andrew Carlos | Ijumaa Wikienda |Over ze weekend

 

FULL VIDEO; Mapambano Ngumi za Global TV – Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania Bingwa

1 Comment
  1. […] karibuni Baraka The Prince ulitangaza kujiondoa kwenye Lebo ya Rock Star 4000 na kuamua ‘kujimeneji’ mwenyewe kupitia Lebo […]

Leave A Reply