The House of Favourite Newspapers

Christian Bella Aacha Historia Mwanza

0

MFALME wa Masauti na Muziki wa Dansi hapa nchini Christian Bella wikiendi iliyopita ameandika historia ya aina yake baada ya kushusha Bonge la burudani kwa mashabiki wake kwenye viunga vya Villa Park Resort vilivyopo Kirumba wilayani Ilemela Jijini hapa.

Msanii huyo mwenye sauti ya kipee pale anapotumbuiza nyimbo zake  hali iliyopelekea mashabiki wake kumbatiza jina la “King of the Best Melody”  alifanikiwa kujizolea umaarufu na kuongeza idadi ya mashabiki wake pale alipoimba nyimbo za Msaliti, Binadamu, Pacha, Nani kama Mama, Ollah, Usilie, Chaku, Pete Subira na nyingine kibao.

 

Katika burudani hiyo iliyoangushwa Wanawake ndio walionekana kukoshwa na nyimbo za msanii huyo hali iliyowafanya wamtunze Vito vya thamani pamoja na fedha katika usiku huo wa burudani uliokuwa wa kipekee jijini Mwanza

 

Na Johnson James- GPL MWANZA

 

 

Leave A Reply