The House of Favourite Newspapers

Chuchu, Ray Kimenuka!

0

DAR ES SALAAM: MSANII wa filamu nchini Chuchu Hans, amezinguana na mzazi mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’ huku chanzo kikidaiwa ni usaliti.

 

Inasemekana kuwa, mkongwe huyo kwenye fani ya uigizaji, amemsaliti Chuchu kwa video queen maarufu Bongo anayefahamika kwa jina moja la Nana.

 

Ishu hiyo ilianza kubumburuka mara baada ya Chuchu kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno ya huzuni, huku akiwalaumu wanaume kwa usaliti wanaoufanya kwa wanawake zao.

Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kuwatafuta wawili hao ili wazungumzie sakata hilo, ambapo kila mmoja alifunguka kivyake.

 

Wa kwanza kutafutwa alikuwa Ray, ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:

“Nipo bize narekodi tamthiliya yangu, naomba unitafute baada ya nusu saa tutazungumza,” alisema Ray ambapo baada ya nusu saa alitafutwa kama alivyoahidi, lakini simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa.

 

Alipotafutwa Chuchu, alithibitisha kuwa kwenye mgogoro na Ray, lakini anashukuru Mungu, kwani amekutana na Malkia wa Taarabu, Khadija Kopa ambaye amemshauri na kumfanya aishi vizuri japo hawako sawa na Ray.

STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI JUMAMOSI

Leave A Reply