The House of Favourite Newspapers

Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-12

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Unajua wewe unakosea kitu kimoja,” alisema mwanamke huyo lakini mara simu ya mume wake ikaita, akaomba kuipokea…
“Pokea baby,” alisema Musa…
“Haloo…”
“Umetoka kazini muda mrefu, umekwenda wapi mama Shua? Niambie ukweli.”
SHUKA NAYO…

Mama Shua alianza kutetemeka, miguu na mikono vilimcheza. Akajikuta akimtumbulia macho Musa baada ya simu kukatwa na mumewe…
“Vipi?” Musa alimuuliza…
“Si unaona. Amepiga simu kazini, akaambiwa nimetoka. Sasa anataka kujua nimekwenda wapi?”
“Amekata simu yeye au wewe?”
“Yeye.”

Mara, simu iliita tena mama Shua akiwa anaongea akaipokea bila kujua ipo hewani, akawa anasema…
“Mi si nilikwambia kuna mtu ofisini anampigiaga simu kumuuliza kuhusu mambo yangu. Atakuwa huyohuyo ndiyo kamwambia mimi nimetoka.”

Baba Shua alisikia yote, hasira zikampanda, akakata simu, akapiga tena. Safari hii ndiyo mama Shua akashtuka baada ya kusikia mlio wa simu yake…
“Subiri nipokee baby,” mama Shua alimwambia Musa.
“Haloo…”

“Uko wapi mama Shua?”
“Nipo saluni, nywele zangu zilikuwa hovyo sana. Ndiyo nimekuja kuziweka sana.”
“Huyo uliyemwambia kuna mtu kazini kwako ndiyo huwa nampigiaga kumuuliza kuhusu mambo yako ni nani?”

Mama Shua alishtuka, akajiuliza ni wakati gani mumewe alisikia, maana ni kweli alisema maneno hayo muda mfupi uliopita akimwambia Musa…
“Si nakuuliza wewe mama Shua?”

“Nilikuwa naongea na huyu dada wa saluni. Aliniuliza kama mumeo amesafiri amejuaje umetoka kazini? Ndiyo nikamwambia kuna bosi wangu huwa anampigia,” alijitetea kwa uongo mama Shua.
“Kwa hiyo bado upo saluni?”

“Ndiyo kwanza huyu dada anamaliziamalizia kuniseti.”
“Naomba niongee naye.”
Mama Shua alipatwa na kiwewe. Alihisi moyo unataka kusimama ghafla. Akajutia akijilaumu moyoni kwamba, angejua angejibu ameshatoka saluni lakini kusema ndiyo kwanza anamaliziwa, ina maana bado yumo saluni, sasa atampa nani simu ili ionekane ndiyo dada wa saluni.

Aliwaza kumkimbizia mtu wa mapokezi lakini akakumbuka ni mwanaume…
“Ayaaa! Da!” alihamaki mama Shua, ikabidi ajibadili mwenyewe sauti, akasema kwa sauti yake…
“Eee shika, mume wangu anataka kuzungumza na wewe.”
Kisha akatumia ya kujibadili…

“Haloo shemu, mambo?”
“Poa, mzima?”
“Mzima. Mi naitwa Zuhura, niko saluni hapa. Mkeo mara nyingi hutumia saluni hii.”
“Oke, sasa…ameondokaje kazini bila kuniambia? Wakati anajua mimi kujua ni rahisi. Hebu mwonye bwana mwanamke mwenzako.”
“Sawa shemeji, nitamwonya. Nadhani ni bahati mbaya tu shemeji.”
“Poa…poa shemeji yangu.”

Baada ya kukata simu, mama Shua alicheka sana mpaka akalala kitandani huku akisema…
“Jamani jamani! Hii dunia hii, balaa.”

“Da! We kiboko aisee. Yaani umenibadilishia sauti hapa mpaka mimi mwenyewe nimekukubali. Kama ningepita hapo nje nisingejua kama ni wewe ndiye uliyekuwa ukiongea kwa sauti hiyo.”
Mama Shua sasa alihisi yuko huru, akambusu Musa kisha akapanda kitandani huku akionekana mwenye furaha sana…

“Unaweza kuendelea au hutaki?” aliuliza mama Shua.
“Nitaweza kweli?” aliuliza Musa…
“Kwangu mimi utaweza tu,” alisema mama Shua huku akimuandaa Musa tayari kwa mzunguko wa pili.
Mama Shua alipeleka mkono na kushika maiki huku akimwangalia mwanaume huyo kwa macho yaliyolegea mpaka Musa akawa ngangari na joto likapanda tayari kwa mpambano.

Musa ndiye aliyeanza kuingia uwanjani akiwa na moto mkali, mwili ulikuwa tayari kwa mechi lakini wasiwsi wa kushindwa kudumu hata kwa dakika tano ulikuwa palepale.
Ile wanaanza mechi tu, mama Shua akaanza kumlaumu Musa…

“Lakini mimi najitoa kwako huku najua kwamba wewe una wanawake wengi sana.”
“Hivi ni kwa nini umeng’ang’ania hilo suala?”
“Nasema kwa sababu najua bwana, usinidanganye.”
“Niamini kweli kabisa.”

“Sikuamini hata kidogo, kwanza nimeshajua iko siku nitajikuta umeniambukiza virusi lakini mimi kama nitakufa itakuwa kwa ajili yako,” alisema mama Shua.
Mazungumzo hayo yalimfanya mama Musa kukosa hali ya kucheza mechi na kujikuta akipitisha madakika bila kumaliza kibarua chake.

Mama Shua alianza kubadilika sauti huku akiendelea kuonga baada ya kuanza kufikia hatua ya mwisho wa mchezo ambapo aliweweseka.
Musa naye, kuona mama Shua yuko kwenye kituo cha mwisho na yeye aliweweseka hadi akajikuta akitaka kupoteza fahamu.
***
Siku za baba Shua kukaa Arusha zilibaki mbili, lakini akarudi nyumbani kwake Dar bila kuzimaliza. Alifika saa kumi na mbili na nusu jioni na kukuta mkewe yuko bafuni anaoga, akachukua simu yake na kukaa sebuleni akaanza kupekua meseji moja baada ya nyingine.

meseji ya kwanza ilikuwa ya mama Shua kwenda kwa Musa, iliandikwa…
“Vipi leo, nahisi kama kuna ulazima. Au wewe unasemaje? Nakusiliza.”
Akafungua majibu ya Musa huku moyoni akisema…

”Huyu Musa huyu…si ndiyo huyu kijana mgeni aliyehamia humu ndani?”
Mara, mkewe akatokea. Alipomwona mumewe ameshika simu yake na anajua mna meseji za Musa, mwanamke huyo huku akiwa amejifunga kanga moja tu, aliruka kama chui na kufika kwenye mwili wa mume wake…
Je, nini kitaendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa, siku ya Ijumaa.

Leave A Reply