The House of Favourite Newspapers

Corona: Waziri Mkuu wa Uingereza Atoka ICU

0

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, ametoka hospitali baada ya kupona maambukizi ya virusi vya corona. Hata hivyo, atalazmika kupumzika kwanza kabla ya kuanza kurejea katika majukumu yake.

 

Johnson, 55, alilazwa St Thomas’ Hospital, mjini London, jana Jumapili – siku ya 10 baada ya kupatatikana na virusi hivyo.

 

Alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku tatu kabla ya kurejeshwa kwenye wodi ya kawaida Alhamisi.

 

Kulingana na taarifa iliyotolewa, kiongozi huyo ataendelea kupumzika katika makazi ya Chequers. Idadi ya watu waliokufa kwa virusi vya corona nchini Uingereza inasemekana kupita 10,000 hadi kufikia Jumapili.

Leave A Reply