The House of Favourite Newspapers

Croatia Yaiangamiza Uingereza, Yatinga Fainali – Video

Timu ya Taifa ya England imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Croatia kwa idadi ya mabao 2-1. Katika mchezo huo, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 na kuamuriwa kuongezwa dakika30 za ziada ili kupata mshindi wa mechi.

 

England walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 5 ya mchezo kwa njia ya mpira wa adhabu uliopigwa na kuwekwa kimiani na Kieran Trippier na baadaye kipindi cha pili Croatia walisawazisha kupitia kwa Ivan Perisic dakika ya 68.

Baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare hiyo, 30 zingine ziliongezwa na Croatia walizitumia vema kwa straika wake, Mario Mandzukic kuandika bao la pili kwenye dakika ya 106.

Mpaka Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo yalibaki kuwa 2 kwa Croatia na 1 kwa England. Kutokana na England kuondoshwa leo, sasa itacheza dhidi ya Ubelgiji kusaka mshindi wa tatu Jumamosi huku Croatia ikiungana na Ufaransa kucheza fainali Jumapili ya wiki hii.

Ni mara moja imewahi kutokea timu ambayo inaongoza mpaka kufikia mapumziko katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia – ikashindwa kufuzu kwenda fainali, mwaka 1990 katika mchezo wa Argentina vs Italy, Argentina waliongoza mpaka mapumziko wakaenda kutolewa mwishoni kwenye penati.

 

Croatia (4-1-4-1): Subasic 7, Vrsaljko 7, Lovren 7.5, Vida 7.5, Strinic 7 (Pivaric 95, 6.5), Rakitic 7.5, Brozovic 7, Rebic 7.5 (Kramaric 101), Modric 9 (Badelj 119), Perisic 8.5, Mandzukic 8(Corluka 116)

Subs not used: Livakovic, Kovacic, Jedvaj, Bradaric, Caleta-Car, Pjaca, Lovren, Kalinic

Goalscorers: Perisic 68, Mandzukic 109

Booked: Mandzukic, Rebic

England: Pickford 9, Walker 7 (Vardy 112), Stones 7, Maguire 7.5, Trippier 8, Alli 7, Henderson 7 (Dier 97, 7), Lingard 6.5, Young 6.5 (Rose 90, 7), Sterling 6.5 (Rashford 74, 7), Kane 7

Subs not used: Butland, Welbeck, Cahill, Jones, Delph, Loftus-Cheek, Alexander-Arnold, Pope

Goalscorers: Trippier 5

Booked: Walker

Manager: Gareth Southgate 7

Referee: Cuneyt Cakir 6

Attendance: 78,011.

 

Highlights 2018 FIFA World Cup Semi-Final Croatia 2-1 England

Comments are closed.