The House of Favourite Newspapers

Dada wa Diamond Atoa Pole kwa Wasanii Walioko Polisi

Esma Platnumz, dada wa Diamond.

WAKATI sakata la madawa ya kulevya linaendelea kuunguruma kila kona ya nchi na kuwajumuisha wasanii maarufu nchini wa Muziki na filamu, Esma ‘Esmaplatnumz’ ambaye ni dada wa nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’,  ameweka ujumbe katika mitandao ya kijamii kuwapa pole watu wa karibu na familia yake wakiwemo marafiki wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na suala hilo.

Baby Taraj.

“Ndugu zetu wa karibu na familia yetu, tunawapenda sana, inshallah Allah atafanya wepesi kwenye jambo hili” ulisema ujumbe huo.

Esma ambaye anatajwa kama mke wa ndoa  meneja maarufu wa wasanii, Petit ‘Petiman Wakuache’, ambaye wanamtoto mmoja wa kike aitwaye Taraj.

 

Picha sambamba na ujumbe wa Esma Instagram

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.