The House of Favourite Newspapers

Daktari Ampiga Stop Aunt

0

DAKTARI maarufu wa magonjwa ya wanawake jijini Dar, amempiga ‘stop’ staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akimtaka kuacha kuzurura, badala yake atulie nyumbani kwa sababu siku za kujifungua zimekaribia hivyo si vyema kuzurura kwenye sherehe mbalimbali usiku.

 

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, daktari huyo anayemhudumia Aunt wakati huu akiwa na ujauzito mkubwa, ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, amesema kuwa, mama anapokuwa mjamzito na siku za kujifungua zikikaribia kama ilivyo kwa Aunt, basi anatakiwa kutulia nyumbani kwani lolote linaweza kutokea na pengine akashindwa kupata msaada wa haraka kutokana na mazingira anayokuwa.

 

 

“Mimi ninamfuatilia Aunt, namuona yupo sehemu mbalimbali za starehe na muda wake wa kujifungua umekaribia. Ni vyema akatulia nyumbani kwa sababu ni jambo jema, anapata muda mzuri wa kupumzika na kutulia, lakini siyo kuhangaika na kichanga tumboni,” anasema daktari huyo.

 

 

Daktari huyo pia aliongeza kuwa angefurahi kuona Aunt anajifungua mtoto salama na mwenye afya kwa sababu kila mama anapenda mtoto wake aliyembeba miezi tisa tumboni, basi atoke salama.

 

 

“Kila mwanamke ana ndoto ya kuona mtoto wake anazaliwa salama bila matatizo yoyote na ndiyo maana hata mimi ninamshauri Aunt atulie, azae mtoto wake salama salimini maana ndivyo kanuni za kidaktari zinavyotaka hivyo,” anasema daktari huyo maarufu.

 

 

Sambamba na hilo, daktari huyo pia alisema kama bado Aunt anatumia pombe hususan kali, aache katika kipindi hiki kwani ni hatari pia. “Nilisoma habari moja mliandika Global kwamba Aunt anatumia pombe, ninamshauri pia hizo aachane nazo kwa sasa kwani siyo nzuri sana kiafya,” alimaliza daktari huyo.

 

 

IJUMAA WIKENDA lilimvutia waya Aunt ili kutaka kumsikia anapokeaje ushauri huo wa daktari, lakini hata hivyo simu yake iliita bila kupokelewa na kwa mujibu wa mtu wake wa karibuni alikuwa amepumzika.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply