The House of Favourite Newspapers

Davido Akacha Mazishi ya Mpiga Picha Wake

0

MSANII maarufu wa Muziki kutoka pande za Nigeria, David Adeleji Adeleke maarufu kama Davido ameingia kwenye headlines baada ya kutoonekana kwenye shughuli ya mazishi ya aliyekuwa mpiga picha wake maalum Fortunate Ateumunname Peter ambaye alifariki dunia Jumanne, Septemba 21, mwaka huu baada ya kuzama mtoni huko Lekki, Lagos.

Fortune amezikwa na watu wachache katika mazishi yaliyohusisha ndugu wa karibu pekee mjini Lagos Nigeria.

Jambo la kustaajabisha lililoibua sintofahamu na kusababisha mijadala mbalimbali mitandaoni ni kitendo cha msanii Davido na timu yake iliyokuwa ikifanya kazi kwa karibu kabisa na marehemu Fortune kutohudhuria kabisa mazishi hayo licha ya marehemu kuwa mtu waliyefanya naye kazi kwa kipindi kirefu mpaka hatua ya mwisho ya uhai wake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio lililopelekea kifo cha Fortune, wanaeleza kuwa chanzo cha kifo chake kilitokana na kusombwa na maji na kisha kuzama katika kina kirefu wakati akijaribu kutafuta kupiga picha bora karibu na eneo la mto wenye kina kirefu uliopo Lekki mjini Lagos Nigeria.

Leave A Reply