The House of Favourite Newspapers

Davina acharuka kisa kurudi kwa mumewe

0

DAVINA11Imelda Mtema

FUNGUKA! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amesema anakasirishwa na ‘wambeya’ ambao kila uchwao wamekuwa wakimuuliza atarudi lini kwa mumewe,  Abdallah Shakoor ambaye walitengana miezi kadhaa iliyopita.

Kuonesha amechoshwa na maswali hayo yanayomfikia kupitia watu wake wa karibu, Davina alisema hakuna mtu anayejua siri yake na siku aliyoondoka aliondoka kwa sababu zake, hivyo siku akiamua kurejea, atafanya hivyo.

“Yaani unamkuta mtu anajadili juu ya mimi kurudi kwenye ndoa yangu na wakati nilivyoondoka hakuna yoyote aliyefahamu hivyo siku ambayo nitaona inafaa kurudi kwenye ndoa yangu, nitarudi na watu watashtukia nimerudi tu mwenyewe bila shuruti ya mtu,” alisema Davina huku akiahidi kuwataja majina wambeya hao kama wataendelea kumsema.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply