The House of Favourite Newspapers

Diamond Akwama Kurejea na Zari Bongo

STORI:Na Musa Mateja | IJUMAA

Msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaduwaza ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea baada ya kutua kutokea Sauzi akiwa peke yake, tofauti na ilivyotarajiwa kuwa angerejea na mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’.

Diamond Platnumzkatika pozi.

Awali zilivuja taarifa kuwa, Diamond amekwenda Sauzi kumchukua Zari na mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni, Nillan ili waje kufanya sherehe kidogo.

Kufuatia taarifa hizo, Jumatatu iliyopita, nyakati za jioni, watu wa karibu na Diamond walifika ‘airport’ kuwapokea lakini kilichowashangaza wengi ni kumuona anatoka mwenyewe na mabegi yake, jambo lililowafanya wahisi kuna kitu.

Mzazi mwenziye na Diamond, Zarina Hassan.

“Hee, mbona yuko peke yake sasa? Zari na watoto wako wapi sasa? Au wamezinguana?” alisikika akisema mmoja wa akinadada waliokuwa uwanjani hapo.

Mbali na dada huyo, wengi walionekana kunong’ona kuonesha kutoamini wanachokiona na kwa kuwa Diamond alijua kuwa kawaangusha kwa kutokuja na Zari, hakuwa na mbwembwe zaidi ya kwenda kwenye gari lililokuwa limeletwa na kijana aitwaye Q Boy, wakaondoka zao.

Diamond.

Katika kujua sababu ya Diamond kutokuja na Zari, mwandishi wetu alijaribu kumpigia simu na kumuuliza kulikoni ambapo alisema: “Mbona kila kitu kiko poa tu, Zari atakuja Bongo wakati wowote.”

Hata hivyo taarifa zilizopatikana baadaye kutoka kwa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake zilieleza kuwa, licha ya ile sherehe ya 40 ya Nillan kubuma Sauzi, kuna mpango wa sherehe kufanyika Bongo Februari 11, mwaka huu na Zari alitarajiwa kutua Bongo siku yoyote kuanzia juzi akiwa na Tiffah na Nillan.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.