The House of Favourite Newspapers

Diamond, Zuchu waacha maswali kwa yasiyo na majibu

0

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Zuhura Othman ‘Zuchu’ aliwaacha mashabiki wake katika maswali baada ya kuingia kwenye onesho lake la ‘mahaba ndi ndi ndi’ akiwa ameshikana mkono na bosi wake, Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kama mtu na mke wake.

Siku chache kabla ya onesho hilo wawili hao walikuwa wakihusishwa kuwepo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Zuchu aliahidi angeweka hadharani mtu ambaye yuko naye na hivyo wengi walitegemea pengine angekuwa ni Diamond, ambaye ilisemekana kuwa anataka kumvalisha pete ya uchumba.

Wasanii hao walifanya sapraizi kwa kuingia pamoja wakiwa kwenye gari la Diamond la Rolls Royce, mwanaume akiwa amevaa mavazi mekundu na mwanamke gauni jeupe refu lenye mpasuo, huku wameshikana mikono.

Muonekano wao, kila mmoja akionesha hisia kwa mwenzake na wakiwa wameshikana kwa tabasamu usoni na furaha watu walidhani kwamba ni wapenzi, lakini baada ya wote wawili kuhojiwa walikana kuwa pamoja.

Katika onesho hilo lililofanyika Mlimani City na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, mashabiki na viongozi wa siasa kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wapendanao juzi, Zuchu alipohojiwa kama huyo ni mpenzi wake alisema ni bosi wake anamheshimu.

Kwa upande wa Diamond alisema: “Zuchu ni msanii wangu na sio mara yangu ya kwanza kuja naye kwenye Zulia Jekundu ‘Red Carpet’, amekua sasa, mara ya kwanza nilimleta hapa mtoto kwa sasa amekuwa msanii mkubwa na mtoto kwa baba hakui.”

Wasanii hao kila mmoja alisema yuko kwenye mahusiano ila hawakuweka hadharani watu wao na kuendelea kuwaacha mashabiki katika maswali.

Leave A Reply