The House of Favourite Newspapers

DIVA: Alikiba Msanii wa Kipekee Tanzania, Mahari Yangu Milioni 500 -Video

0
Msanii na mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Malinzi  ‘Diva The Bawse’ akifanya mahojiano na Bongo 255.

MSANII na mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Malinzi  ‘Diva The Bawse’ leo  Jumatano Januari 22, 2020,  amefanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio iliyopo katika jengo la Global Group Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Katika mahojiano yake amesema anavutiwa na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba,  huku akisema anavutiwa na kipaji chake na jinsi anavyofanya kazi zake bila kujitangaza kupitia vyombo vya habari kama alivyozindua msikiti bila kuwaita watu wa  ‘media’.

 

”One and only Alikiba is the most talented artist in the nation, ana mwenbwe hatengenezi watu kumshangilia au watu wa kamera kumpokea akienda sehemu.  Anaishi maisha yake, sauti yake ipo ‘powerful’ akimalizia kuimba wimbo wake wa Mshumaa,’‘ alisema Diva.

…Diva akiwa na watangazaji wa kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio.

Diva amesema yeye ndiye mtu ambaye alimfanya msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Tekno Miles,  kujulikana nchini Tanzania huku akisema alipokuja nchini Tanzania aliogopa kwenda kumuona kutokana na kutopenda maneno ya watu. 

Pia amefunguka kuwa hapendi kuweka wazi mambo yake ya mahusiano,  na akitokea mtu wa kumuoa atalazimika kutoa Shilingi milioni 500 kwa kuwa kuna vitu vingi ambavyo amevifanya kufikia hapo alipo kwa sasa,  akiwaomba Watanzania kufanya mambo yao kuliko kufuatilia maisha yake.

Hata hivyo, mtangazaji huyo amegoma kumzungumzia mwanamuziki Diamond Platnumz katika mahojiano hayo.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiongea jambo na Diva.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, akiongea na Diva.
Diva akikabidhiwa gazeti la Championi Jumatano Mhariri wa Championi Jumamosi, Lucy Mgina.
…Akipewa gazeti la Risasi Mchanganyiko na Mhariri wa gazeti hilo Erick Evarist.

 

Leave A Reply