The House of Favourite Newspapers

Diva Kumburuza Gigy Kortini

0

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ amefunguka kuwa, atamburuza kortini msanii Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kutokana na maneno anayomtukana mitandaoni.

 

Kwa takriban wiki mbili sasa, Diva na Gigy wamekuwa wakirushiana maneno mazito mitandaoni na Risasi Jumamosi lilipomtafuta Diva kutaka kujua kiini cha ugomvi wao, alieleza kusudio lake la kumpeleka Gigy mahakamani.

 

“Sitaki hata kumzungumzia Gigy, lakini nitapambana naye na sijawahi wala sitaki kuwa na mazoea naye, nilikutana naye mara moja kipindi anafanya kazi na Soudy Brown alipokuwa anatambulisha muziki wake na kwa kuwa Soudy ni rafiki yangu, aliniomba nimpe sapoti msanii wake. Kuhusu bifu naye, kwa sasa hii ishu iko kwa mwanasheria wangu na atamshughulikia nadhani atakapofikishwa mahakamani ataniheshimu,” alifunguka Diva.

 

Risasi Jumamosi lilimtafuta Gigy ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo, lakini simu yake haikupatikana.

STORI: Irene Marango

MAHUBIRI YA MAMA RWAKATARE – “KUPATA MWANAUME NI BOMU”

Leave A Reply